Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safaricom yapata faida ya Tsh. Bilioni 762

Saf Safaricom half-year profit rises to Sh37bn on end of free M-Pesa

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Safaricom imefanikiwa kupata faida ya zaidi ya Tsh. Bilioni 700 kwa mauzi ya nusu mwaka hadi kufikia September 30, faida ambayo inatajwa kuchangiwa na mapato ya miamala ya M-Pesa baada ya kuondolewa makato utumaji na upokeaji pesa.

Safaricom sasa imetangaza ongezeko la 12.1% kwenye makusanyo yake kutoka shilingi za Kenya Bilioni 33 zilizopatikana mwaka uliopita ambapo kumekua na ongezeko la miamala ya simu kwa asilimia 45.8 mpaka kufikia makusanyo ya zaidi ya Tsh. Trilioni 1.071.

Mwezi December mwaka 2020 Benki Kuu ya Kenya (CBK) ilifuta tozo za miamala kwenye utumaji na upokeaji pesa chini ya shilingi za Kenya 1000 ili kukabiliana na athari za maambukizi ya COVID-19

Chanzo: www.tanzaniaweb.live