Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za Kenya kupinga wazo la Rais Biden

Bidwen Pic Sababu za Kenya kupinga wazo la Rais Biden

Thu, 14 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya imekataa kuunga mkono mpango la Rais Biden wa kushinikizza punguzo la ushuru kwenye kampuni za kimataifa na kusema kuwa utawazuia kukusanya mapato kutoka kwa kampuni kubwa za teknolojia kama za Google, Facebook na Amazon.

Mkutano Mkuu wa Uchumi na Maendeleo OECD, uliofanyika mjini Paris ulijadili kuhusu nafuu ya ushuru kwa kampuni hizo za kimataifa na ndipo walipobainisha kuwa Kenya haipo kwenye orordha ya nchi 136 zilizokubali kupitisha wazo hilo.

Nayo Mamlaka ya Mapato nchini Kenya KRA, imethibitisha kuwa nchi hiyo haikuridhishwa na makubaliano hayo ambayo yatailazimisha kutupilia mbali kodi ya asilimia 1.5 kutoka kwa kampuni hizo.

"Kwa mataifa yatakayo kubaliana wazo hilo basi yatalazimika kutupilia mbali kodi za kampuni hizo, hii haijaka sawa kwetu" Amesema Terra Saidimu Afisa wa KRA.

KRA imeongeza kusema kuwa kukubali kutia saini pendekezo hilo kutakwamisha miango ya makusanyo ya mapato ya Shilingi bilioni 13.9 za kitanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live