Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SIO ZENGWE: Ahmad Ahmad amerahisisha kufuzu, tunafanya nini

Zengwe Pic Data SIO ZENGWE: Ahmad Ahmad amerahisisha kufuzu, tunafanya nini

Tue, 2 Mar 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

Moja ya mambo ambayo rais wa sasa wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad amerahisisha ni kufuzu kwa fainali za mashindano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) na mashindano yote yanayohusu umri, isipokuwa fainali za AFCON ambazo kuna wakati huunganishwa na michuano ya awali ya Kombe la Dunia.

Kwa kawaida ratiba ya michuano ya kufuzu kwa fainali za michuano ya Afrika huzingatia nafasi ya nchi katika orodha ya ubora ya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), ndio maana awali ilikuwa ngumu sana kufuzu. Ilikuwa ngumu kwa sababu raundi ya kwanza unaweza kupata nchi kibonde mwenzako lakini raundi ya pili ukatwishwa Nigeria, Morocco au Misri.

Hapo ndipo panakuwa mwisho wa safari yako na ndivyo inavyoendelea kuwa katika mashindano mengine yasiyo ya umri kama Kombe la Dunia na AFCON.

Lakini katika kuwarahisishia viongozi wa vyama vya soka vya nchi ambao walikuwa wakiona kuwa mfumo huo hauleti uwiano wa uwakilishi wa kanda katika fainali hizo, na bila shaka kutumia siasa kuendelea kujichimbia CAF, Ahmad alilegeza mchakato wa kufuzu kwa mashindano ambayo ana uwezo nayo kwa kiasi kikubwa.

Sasa kufuzu kwa fainali za U-17, U20 na CHAN ni mwendo wa kanda. Unatafuta tikewti yako kwenye kanda. Yaani kwa kanda yetu unaweza kukutana na Burundi, Djibout na Sudan Kusini ukawa umemaliza mechi zako na tiketi mkononi.

Au timu zikashindana katika kanda, kama CECAFA na zile zinazofika fainali zinakjuwa zimeshafuzu kucheza michuano ya Afrika. NI kurahisisha mchakato kupita kiasi na hoja kubwa inakuwa kwamba kila kanda imepata uwakilishi sawa, lakini kiwango cha mashindano kinashuka kwa sababu zile juhudi za kanda fulani kupandisha kiwango chake na hivyo kuwa na timu nyingi zilizo juu katika orodha ya ubora, zinapunjwa nafasi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz