Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yashika nafasi ya 4 kuvutia uwekezaji Afrika

Rwanda Invst Rwanda yashika nafasi ya 4 kwa uwekezaji Afrika

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rwanda imeshika nafasi ya nne katika orodha ya mataifa yanayoongoza kwa kuvutia uwekezaji barani Afrika kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Rand Merchant Bank, RMB.

Benki hii ya ushirika inaongoza kwa kufanya uwekezaji barani Afrika, huku ikiwa nafasi ya kwanza kwa taasisi za kifedha barani humu.

Katika ripoti waliotoa mwaka 2021 kwa nafasi 10 za nchi zinazovutia uwekezaji Afrika, wametaja sababu zinazopelekea kuwepo kwa hali hiyo ya kuvutia huku wakimulika suala la mazingira rafiki ya kuwekeza pamoja na sera za mamendeleo zinazo tekelezeka.

Hata hivyo, Rwanda ilikuwa nafasi ya tisa katika ripoti zilizopoita, hivyo hatua hii ina ashiria kukua kwa uchumi wa nchi hiyo.

Nafasi ya kwanza imeshikiliwa na Misri, huku Morroco wakishika nafasi ya pili na Afrika Kusini ikiwa nafasi ya tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live