Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yaanza kutumia Pikipiki za umeme zilizotengenezwa nchini humo

Rwanda Motorgettingpassengernyamirambo Rwanda yaanza kutumia Pikipiki za umeme zilizotengenezwa nchini humo

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa miaka 12 Didier Ndabahariye amekuwa akiwasafirisha wateja wake katika barabara za mji wa Kigali -yeye ni mmoja wa maelfu ya wandesha piki piki za kibiashara, wanaofahamika kama motos.

Hivi karibuni aliachana na pikipiki yake ya kawaida na kugeukia ile ya umeme kuendesha shughuli zake katika mji mkuu wa Rwanda ikiwa ni moja ya piki piki za kwanza za umeme barani Afrika.

"Siku za kwanza, mambo hayakua mazuri kwa sababu nilikua sijazoea kuendesha e-motos na wakati mwingine piki piki inazima.

"Hata hivyo niliendelea na kazi, na baada ya siku chache nikajifunza mambo mengi kuhusu vile inavyofanya kazi na jinsi ya kuendesha. Ndipo nikaanza kupata pesa na kuweka akiba zaidi," Didier anaelezea.

Yeye ni mmoja wa waendesha piki piki 60 wa piki piki za umem kutoka kampuni ya Rwanda ya Ampersand.

Kuna karibu pikipiki 25,000 zinazohudumu kama texi katika mji mkuu wa Rwanda

"Sasa nazipenda pikipiki hizi - za umeme maarufu e-motokwani inauwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu bila kukumbwa na na matatizo ya kiufundi ukilinganisha na zile zilizo na injini - na inaenda vizuri, pia ni rahosi kuendesha."

Mradi huo wa kwanza wa kampuni ya Ampersand una malengo ya kuhakikisha piki piki zote nchini Rwanda zitakua za umeme katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Kuna karibu piki piki 25,000 zinazohudumu kama teksi mjini Kigali,zingine zinaendeshwa kwa hadi saa 10, nahuwa zinasafiri mamaia ya kila mita kila sik.

"Pikipiki ni nyingi kuliko magari katika eneo hili la ulimwengu,"anasema Afisa Mkuu Mtendaji wa Ampersand Josh Whale.

"Injini zake ni rahisi na hazina aina ya teknolojia ya gharama kubwa ya kupunguza uzalishajiwa hewa chafu unayona kwenye magari ya kisasa. Pia zinaendeshwa kwa zaidi ya kilo mita 100 kwa siku, Hivyo basi kuchangia uchafuzi wa mazingira kutokana na uzalishaji wa hewa ya kaboni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live