Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rungu la FIFA latua kwa Sofapaka ya Kenya

 117536667 182983711 FIFA yaiadhibu Sofapaka

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Kabumbu Duniani – FIFA limeifungia klabu ya Sofapaka inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya kutofanya usajili wa wachezaji wa kimataifa na kuliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya – FKF kuizuia timu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani kwa kushindwa kulipa madeni wanayodaiwa na mchezaji wao wa zamani.

Rungu la FIFA linakuja kufuatia kusitisha mkataba na mshambuliaji kutoka Ghana, Jedinak Nana Ameyaw kwa madai kuwa mchezaji huyo hakuwa na kiwango kizuri.

Sofapaka ilisitisha mkataba wa mchezaji huyo mwezi Januari mwaka huu 2021.

Mchezaji huyo aliyekuwa amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo alikata rufaa kupitia Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa cha Ghana akitaka alipwe mishahara ya muda uliosalia katika mkataba wake.

Kwa mujibu wa FIFA, adhabu iliyowasilishwa kwa Sofapaka Jumatatu (Desemba 06) itakoma pale tu mchezaji huyo atakapolipwa stahiki zake.

Rais wa klabu hiyo Elly Kalekwa amenukuliwa na BBC akisema: Tuna kila aina ya dhamira ya kumlipa fedha zake haraka iwezekanavyo.

Kinachokwamisha ni changamoto ya fedha tuliyonayo kwa sasa”.

Kalekwa ameongeza kuwa klabu hiyo inatarajai kumalizana na deni hilo ifikapo Januari mwaka 2022.

Ameyaw anaidai Sofapaka FC $12,000 sawa na shilingi za kitanzania milioni 26 za mshahara wa mwaka mmoja na nyongeza ya $1,000 (TZS milioni 2) za gharama za kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live