Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robo fainali Caf ni vita ya pesa

054741b745f1b31b457806132c87db51.jpeg Robo fainali Caf ni vita ya pesa

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MJADALA unaoendelea hivi sasa katika vyombo vya habari ni hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo jumla ya klabu nane zinaenda kuoneshana umwamba.

Simba kutoka Tanzania ni miongoni mwa timu zilizofuzu hatua ya robo fainali kwa kishindo baada ya kuongoza Kundi A, ambalo lilikuwa na miamba kama Al Ahly, El Merrikh na AS Vita.

Kuingia katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika sio jambo rahisi hata kidogo linahitaji uwekezaji mkubwa pamoja na wachezaji wa daraja la juu ili kutoa upinzani na kuongeza msisimko wa mashindano.

Hiyo haishangazi kuona baadhi ya klabu kuwa na mchezaji mwenye thamani kubwa mfano miamba kama Al Ahly, ambayo mlinda mlango wake Mohamed El Shenawy ana thamani ya Euro milioni 2.25 sawa na Ferjani Sassi mshambuliaji wa kati wa Zamalek ambao ndio nyota ghali zaidi barani Afrika.

Lakini pia Kaizer Chiefs, ina nyota ghali kama Khama Biliat, ambaye ana thamani ya Euro milioni 1.35 uwekezaji huu umekuwa chachu kwa klabu hizi kufanya vyema katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na uwekezaji wake.

Leo nakuletea gharama za vikosi vya klabu, ambazo zimetinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

AL AHLY EURO MIL 25.5

Miamba hii kutoka nchini Misri ndio klabu yenye kikosi ghali zaidi, ambacho kinagharimu Euro milioni 25.5 ambazo ni sawa na Sh bilioni 70.44 imeingia katika hatua ya robo fainali kutokea Kundi A kama mshindi wa pili wakiwa wamejikusanyia pointi 11 nyuma ya Simba,

ambayo ilimaliza hatua ya makundi ikiwa na pointi 13.

MAMELODI EURO MIL 18.9

Vijana wa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Patrice Motsepe, wanashika nafasi ya pili katika orodha ya klabu zenye kikosi ghali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa, ambapo timu yao ina thamani ya Euro milioni 18.9 (sawa na Sh bilioni 52.43)

Timu hiyo imetinga hatua ya robo fainali wakiwa vinara wa Kundi B wakihitimisha hatua ya makundi kileleni baada ya kujikusanyia pointi 13.

ESPERANCE EURO MIL 17.90

Mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Tunisia wanashika nafasi ya tatu kwa klabu zenye

kikosi ghali hatua ya robo fainali, ambapo timu yao inagharimu Euro milioni

17.9 (sawa na Sh bilioni

49.45).

Wababe hao wametinga hatua ya robo fainali wakitokea kundi D, ambapo wamemaliza wakiwa vinara baada ya kujikusanyia pointi 11.

WYDAD EURO MIL

13.3 Hii ni miamba mingine kutoka Afrika Kaskazini timu anayocheza kiungo mshambuliaji wa Tanzania, Saimon Msuva ni miongoni mwa timu tishio zenye vikosi ghali, ambapo wanashika nafasi ya nne kikosi chao kikiwa na thamani ya Euro milioni

13.3 (Sawa na Sh bil 36.74).

Simba hao wa Milima ya Atlas wamefuzu hatua ya robo fainali wakiwa vinara wa Kundi C, ambapo

walimaliza wakiwa na pointi 13.

KAIZER CHIEF EURO MIL 11.08

Miamba mingine kutoka nchini Afrika Kusini inashika nafasi ya tano katika orodha ya timu ghali zilizofuzu hatua ya robo fainali licha ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kufanya usajili baada ya kumsajili Andriamirado ‘Dax’ Andrianarimanana, walioufanya 2018 akitokea Fosa Juniors ya nchini Madagascar.

Bado kikosi chao ni ghali kina thamani ya Euro milioni 11.08, ambazo ni sawa na Sh bilioni 30.60 wametinga hatua ya robo fainali wakitokea Kundi C.

CR BELOUIZ EURO MIL 10.93

Mabingwa watetezi wa

taji la Ligi Kuu ya Algeria ni klabu inayoshika nafasi ya sita katika timu zenye vikosi ghali, ambapo kikosi chao kina thamani ya Euro milioni 10.03 (Sawa na Sh bilioni 27.70).

Timu hiyo imeiongia hatua ya robo fainali wakitokea Kundi B wakishika nafasi ya pili nyuma ya Mamelodi Sundowns, ambapo wamejikusanyia pointi tisa.

MC ALGIERS EURO MIL 7.90

Wakali wengine kutoka Ligi Kuu ya Algeria ni timu inayoshika nafasi ya saba katika orodha ya timu ghali zilizofuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kikosi chao kikiwa na thamani ya Euro milioni 7.90 (Sawa na Sh bilioni 21.82).

Timu hiyo imetinga hatua ya robo fainali iki-

tokea Kundi D ikikamata nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi tisa.

SIMBA SC EURO MIL 2.2

Wawakilishi wa Tanzania katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ndio wanakamilisha orodha kwa kushika nafasi ya mwisho kwakuwa na kikosi ghali, ambapo timu yao ina thamani ya Euro milioni 2.2 (Sawa na Sh bilioni 6.07).

Timu hiyo pamoja na kuwa na kikosi chenye gharama ndogo ukilinganisha na timu zingine zilizofuzu nane bora, lakini ni moja ya timu zilizofanya vizuri zaidi katika hatua ya makundi.

Walicheza katika Kundi A na walimaliza wa kwanza wakiwa na pointi 13, mbili mbele ya mabingwa watetezi, Al Alhy.

Chanzo: www.habarileo.co.tz