Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi ndege za Kenya kufanya safari NewYork

Kq Dreamliner Rasmi ndege za Kenya kufanya safari NewYork

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bunge la nchini Kenya limeunga mkono uamuzi wa Baraza la Mawaziri wa kurekebisha makubaliano ya huduma za anga kati ya taifa hilo na Marekani ambao utaongeza safari katika mji wa New York.

Kwasasa shirika la ndege la nchini humo KQ, lipo kwenye mchakato wa kupanga safari kwa wasafiri kutoka katika Mji Mkuu wa Nairobi hadi NewYork.

Mnamo Februari 5, mwaka 2020 Kenya ilisaini makubaliano na Marekani ikipendekeza kurejelewa kwa makubaliano ya usafiri wa anga yaliyofanyika Washington DC Juni 08, 2008.

Mkataba huu pia utaruhusu mashirika ya ndege ya Kenya kufanya safari za Marekani sambamba na kukuza biashara kwa pande zote mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live