Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rapa King Kaka azungumzia hali yake ya kiafya baada ya kuugua kwa miezi mitatu

876bf32441c9a2ac Rapa King Kaka azungumzia hali yake ya kiafya baada ya kuugua kwa miezi mitatu

Sun, 12 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rapa King Kaka amewataka mashabiki wake wafurahie na kutunza afya zao baada ya yeye kulazwa kwa muda wa miezi mitatu hospitalini bila madaktari kutambua ugonjwa aliokuwa akiugua.

King Kaka amesema kwamba amepoteza kilo nyingi kutokana na ugonjwa ambao hadi kufikia sasa madaktari hawajabaini ni upi ila ana matumaini kwamba atapata nafuu. King Kaka amesema alionesha dalili za virusi vya COVID-19 lakini alipopimwa hakupatikana navyo.

Rapa maarufu na mfanyabiashara Robert Ombima almaarufu King Kaka ambaye amekuwa akiugua kwa muda mrefu amezungumzia hali yake ya kiafya.

Kupitia kwenye ujumbe wake kwenye mtandao wa Facebook, King Kaka aliwarai mashabiki wake kufurahia afya njema kwani alilazwa kwa muda wa miezi mitatu hospitalini bila madaktari kutambua ugonjwa aliokuwa akiugua.

" Kusema ukweli dari za hospitali hazipendezi ukizitizama kila siku, shukuru Mungu kwa afya njema, Kinga Kaka alisema huku akiwahakikishia mashabiki kwamba anaendelea kupata nafuu.

Mapema mwezi Septemba, King Kaka alifichua kwamba amepoteza kilo nyingi kutokana na ugonjwa ambao kufikia sasa hawajabaini ni upi ila ana matumaini kwamba atapata nafuu.



Baada ya kuondoka hospitalini, King Kaka alisema alionyesha dalili za virusi vya COVID-19 lakini alipopimwa hakupatikana navyo.

Msanii huyo pia alisema alikuwa amepoteza hamu ya kula na alikuwa akilazimishwa tu kunywa uji na matunda.

" Mashabiki wangu , nimeonelea niwafahamishe hili, nimekuwa mgonjwa kwa miezi mitatu na siku nane, nimepoteza kilo 33 kwa sasa, hakuna ugonjwa uliopatikana baada ya kupimwa, nimekuwa nikienda hospitalini kila mara, la kushangaza sihisi uchungu mahali popote, nina matumaini kwamba tutapata suluhisho hivi karibuni, kwa sasa hata sina nguo nimekonda sana, sina hamu ya chakula hata kidogo," Alisema King Kaka.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke