Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Ruto amteua Gavana Joho kuwa Waziri wa Madini

JOHO 2 Mn Gavana wa Mombasa, Hassan Joho.

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya, William Ruto ametangaza kundi la pili la Baraza la Mawaziri lenye Mawaziri ambao wameungana na wenzao 11 ambao waliteuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo miongoni mwa walioteuliwa yumo Gavana wa Mombasa, Hassan Joho ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Madini na Uchumi wa Bluu.

Baadhi ya Wanachama kutoka Vyama vya Upinzani ambao wameteuliwa katika Serikali ya Ruto ni Joho kutoka Chama cha ODM cha Raila Odinga na Mbunge John Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha, aliyekuwa Gava wa Kakamega Wycliffe Oparanya ameteuliwa kuongoza Wizara ya Vyama vya Ushirika.

Wengine walioteuliwa ni aliyekuwa Waziri wa Utalii katika Baraza la Mawaziri lililovunjwa Alfred Mutua ambaye amerudishwa kuwa Waziri wa Kazi na Jamii, huku Wycliffe Oparanya akielekea katika Wizara ya Maendeleo ya MSME.

Wakati huohuo, Justin Muturi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, ameteuliwa kuongoza Wizara ya Utumishi wa Umma, huku Stella Lagat akiwa katika Wizara ya Jinsia, Utamaduni na Sanaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live