Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi mstaafu awaongoza majambazi waongozwa kuvamia na kuiba, CCTV yanasa kila kitu

Majambazi Mstaafuuu Tukio lilivyotokea

Thu, 16 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi nchini Kenya limesema majambazi sita waliokuwa wamejihami kwa bunduki na mapanga kisha kumvamia mwanamke mmoja akiingia nyumbani kwake mtaani Gataka, Rongai, walioongozwa na afisa wa polisi mstaafu (hajatajwa jina) kutekeleza unyama huo.

Katika video iliyosambaa mitandaoni mwishoni mwa wiki iliyopita, inawaonyesha majambazi hao wakimvamia mwanamke huyo aliyekuwa ndani ya gari lake kisha kupasua kioo cha mlango wa upande wa dereva na kumwamuru kutoka na kuwapa pesa. Waliingia naye mpaka ndani mwake wakampiga na kuchukua pesa.

Baada ya kutekeleza tukio hilo, majambazi hao walitokomea kusikojulikana pasi na kujua kwamba katika eneo walilokuwa wakifanya unyama huo, kulikuwa na CCTV kamera ambazo zilinasa tukio zima mwanzo hadi mwisho.

Aidha, polisi imesema imewakamata washukiwa wawili wa tukio hilo huku mmoja akikamatwa katika kibanda cha Mpesa akijaribu kutoa pesa kiasi cha Ksh 240,000 (sawa na Tsh ) katika eneo la Kasarani, na tayarin alikuwa ameshatoa Ksh 240,000 nyingine. Mhudumu wa Mpesa ambako pesa hizo zilitolewa naye alikamatwa na kuhojiwa.

Kufuatia uvamizi huo, Waziri wa Usalama, Fred Matiang’i alitembelea eneo la tukio akiwa ameambatana na Inspekta Jenerali wa Polisi, Hilary Mutyambai na Mkuu wa Kitengo cha Huduma Maalum katika Idara ya Upepelezi wa Jinai, (DCI) Pius Gitari na kuwahakikishia wakaazi kuwa hatua madhubuti zitachukuliwa.

Ziara ya viongozi hao pia ilidhamiria kufahamu hali halisi ya usalama eneo hilo, kukiwa na malalamiko ya wakaazi ambao wamesema kuna changamoto ya kudorora kwa usalama na kuhimiza polisi kuchukua hatua.

Tazama video ya tukio hilo.

View this post on Instagram

A post shared by Tanzania Web (@tanzaniaweb)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live