Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Kenya watoa onyo kali kwa waandamaji (+Video)

Video Archive
Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja Kirocho ameonya waandamanaji siku ya Jumanne kutojaribu kuingia katika maeneo yanayolindwa na serikali huku maandamano ya kuipinga serikali yakiendelea.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Kanja amesema kuwa ripoti za ujasusi zinaonyesha kuwa maandamano ya sasa yamesheheni vitendo vya fujo vinavyotekelezwa na wahalifu.

"Kulingana na duru za kuaminika, maandamano ya sasa yamegeuzwa kimbilio la wahalifu, walio na ari ya kupora na kuharibu mali ya Wakenya wachapakazi,"

Afisa huyo alikuwa akizungumza dhidi ya wito wa vijana wa Kenya kutaka kuingia katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta International Airport kupinga utawala wa Ruto.

"Polisi inasisitiza kwamba maeneo yaliyohifadhiwa hayafai kuingiliwa ikama livyoainishwa katika Sheria ya Maeneo yaliotengwa."

Kulingana na afis huyo wa polisi, maeneo yote yaliyotengwa, ikiwa ni pamoja na mitambo ya LPG na Bitumen na mabohari ya petroli katika eneo la Embakasi , Uwanja wa ndege wa JKIA, hayapaswi kuingiwa na watu wasioruhusiwa.

Aliendelea kusema kuwa Sheria ya Usafiri wa Anga ya Kenya inasema ni kinyume na sheria kuingilia ardhi yoyote ambayo ni sehemu ya uwanja wa ndege wa serikali. "Haitakubalika kuingia kwa Uwanja wa ndege ikiwa huna ruhusa, hiyo haitakubalika," alisema mkuu huyo wa polisi .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live