Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Odada, Kinda anayemfukuzisha wanyama Harambee Stars

Richard Odada Kinda Richard Odada

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama kiungo Victor Mugubi Wanyama bado ana matumaini ya kuichezea tena timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, basi aombe dua kocha Jacob Ghost Mulee aachane na kikosi hicho.

Hii ni baada ya Mulee kutoa kauli kwamba hana nia wala mipango ya kumtumia Wanyama akisisitiza kuwa muda wake umekwisha.

Toka alipoteuliwa kwa mara ya tatu kuwa kocha wa Harambee Stars, Oktoba 2020, Ghost hajawahi kumwita hata mara moja kikosini Wanyama.

Mara kadhaa amekuwa akijitahidi kukwepa maswali kuhusu ni kwa nini hamwiti kikosini Wanyama ambaye alikua nahodha wa timu hiyo.

"Nilipoichukua timu (kutoka kwa Francis Kimanzi), tukiwa tunajiandaa na mechi dhidi ya Comoro na Togo, sikumkuta Wanyama kwenye kikosi nilichorithi. Ndicho kipindi nilichoamua lazima kuwe na mabadiliko na nikamteua Olunga kuwa nahodha mpya wa timu." amesema Mulee

Hii sasa ina maana kuwa career ya Wanyama na Stars huenda ikawa imefikia kikomo na ikiwa ana matumaini ya kuvalia jezi za taifa tena, basi itakuwa ni chini ya kocha tofauti na sio Mulee

Lakini hata ikitokea akaja kocha mwingine, itakuwa vigumu sana Wanyama kupata nafasi tena hasa baada ya mrithi wake kupatikana akiwa ni mchezaji chipukizi Richard Odada.

Odada anayecheza soka lake la kulipwa kule Serbia katika klabu ya Metalac GM, amecheza kwenye mechi yake ya kwanza ya kimataifa dhidi ya Uganda Cranes na kuonyesha kiwango kikubwa kilichowafurahisha mashabiki na wachambuzi wengi, licha ya mechi hiyo kuishia kwa sare tasa.

Mulee alimpa mechi yake ya pili ya kitaifa dhidi ya Rwanda juzi Jumapili iliyomalizika kwa sare nyingine ya 1-1.

Odada mwenye miaka 21, alitisha akicheza kama kiungo mkabaji nafasi aliyokuwa akicheza Wanyama.

"Nafikiri chipukizi Odada kaonyesha kiwango kizuri katika mechi hizi na ukiniuliza mimi, tatizo tulilokuwa nalo la kiungo mkabaji, sasa tumelitatua. Kwa muda mrefu sijawahi kuona kiungo mkabaji kama Odada hapa Afrika. Alikamata aeneo la kati vyema, alitoa pasi za umakini zilizomfikia mlengwa na stamina yake ni ya ajabu. Hatuna tatizo tena kwenye safu ya kati." amesisitiza Mulee

Wanyama aliyeichezea Stars mechi 60, alikabidhiwa unahodha wa Harambee Stars na kocha Mbelgiji Adel Amrouche akimrithi straika mstaafu Dennis Oliech.

Wanyama aliewika EPL akiwa na Southampton na Tottenham Hotspurs kwa sasa anakipiga katika klabu ya CF Montréal ya Ligi kuu nchini Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live