Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ODM haijajiunga na serikali ya Ruto - Katibu mkuu wa chama cha ODM Kenya

ODM Haijajiunga Na Serikali Ya Ruto   Katibu Mkuu Wa Chama Cha ODM Nchini Kenya.png ODM haijajiunga na serikali ya Ruto - Katibu mkuu wa chama cha ODM Kenya

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Katibu Mkuu wa chama cha ODM nchini Kenya Edwin Sifuna ameshikilia kuwa chama hicho hakijajiunga na serikali ya Rais William Ruto.

Bw Sifuna ameyasema hayo baada ya Rais William Ruto kuwateuwa viongozi 4 wa ODM kujiunga na serikali yake.

Akizungumza siku ya Alhamisi, Sifuna alisema kuwa hakuna uamuzi wowote ambao umefanywa na chama wa kujiunga na serikali ya Rais Ruto.

"Ukweli wa mambo ni kwamba hakuna uamuzi wa chombo chochote cha ODM kinachojiunga na serikali ya Ruto."

Aliendelea kusema kuwa kumekuwa na juhudi za kukipaka matope chama cha ODM tangu kinara wa chama Raila Odinga alipohudhuria hafla ya kutiwa saini kwa Mswada wa mageuzi katika Tume ya Uchaguzi (IEBC) kuwa sheria.

Sifuna alivishutumu vyombo vya habari kwa kupotosha msimamo wa chama cha Chungwa kuhusu suala hilo.

Chanzo: Bbc