Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niyonzima, Lamine watamba kimataifa

Niyonima Kigali Kiungo wa AS Kigali, Haruna Niyonzima

Sun, 19 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Yanga kiungo Haruna Niyonzima na beki kisiki Lamine Moro wametamba kimataifa baada ya kuiwezesha timu yao ya AS kigali kufuzu raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Kigali imefuzu kwenye raundi ya kwanza kwa kuibamiza Missiri ya Comoro kwa ushindi wa jumla wa mabao 8-1.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza ambao Kigali ilicheza ugenini iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 kisha katika mkondo wa pili uliochezwa leo nchini Rwanda imetoa kipigo kizito cha mabao 6-0.

Mechi nyingine za michuano hiyo ilikuwa ni pamoja na FAR Rabat ya Morocco iliyoitoa Buffles du Borgou ya Benin, Red Arrow ya Zambia ikaitoa Young Buffaloes ya Eswatin, Orapa United ya Botswana ikiwa nyumbani ikaifunga Mangasport ya Gabon na kupita wakati Bumamuru ya Burudni imetolewa na Diables Noiris ya Congo.

Police ya Nigeria ikaifunga pingu Ben Guerdane ya Tunisia na mchezo wa mwisho ulikuwa kati ya wanajeshi wa mpakani, Biashara United ya Mara iliyoiondoa Dhikil ya Djibout.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live