Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndoa ya Rude Boy matatani

Rude Boy Msanii wa Nigeria , Paul Okoye

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

Ndoa kati ya mwanamuziki Paul Okoye ‘Rude Boy’ na Anita Okoye imeripotiwa kupitia misukosuko kiasi cha mke wake huyo kuwasilisha ombi la talaka Mahakamani huko Abuja, Nigeria hivi karibuni.

Taarifa za anguko la ndoa hiyo zimekuwa kubwa baada ya nyaraka za talaka zilizowasilishwa Mahakamani na Anita kuvuja mitandaoni.

Paul na Anita Okoye wana watoto watatu (3) na imeelezwa kuwa pande zote mbili zitaendelea kutoa matunzo bora kwa maslahi ya watoto wao ambao kwasasa wanaishi Marekani.

Wawili hao wamekuwa pamoja kwa karibu miaka 17, na wamedumu kwenye ndoa kwa miaka 7.

Chanzo: eatv.tv