Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndani ya siku 304, Diaspora wametuma Tsh. Bilioni 700 kuingia Kenya

Ssdsfdkf Ndani ya siku 304, Diaspora wametuma Tsh. Bilioni 700 kuingia Kenya

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakenya wanaoishi nje ya nchi wametuma pesa nchini humo wastani wa Tsh. bilioni 49 kwa mwezi, huku wale wanaotumia benki kutuma pesa taslimu, wakilipa zaidi ikilinganishwa na zile zinazotumia njia za kidijitali.

Benki Kuu ya Kenya (CBK) imesema gharama ya kutuma pesa kwa Kenya ni wastani wa takriban asilimia saba, ambayo ni chini kidogo ya wastani wa asilimia nane kwa Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahara lakini zaidi ya shabaha mwafaka ya asilimia tatu.

Katika muda wa miezi 10 hadi Oktoba 2021, Wakenya wanaoishi nje wametuma nyumbani wastani wa Tsh. Bilioni 700, kiwango ambacho ni asilimia 20.4 ikilinganishwa na Sh28.5 bilioni zilizotumwa katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

"Suala la gharama ni wasiwasi mkubwa, sio tu kwa Kenya lakini kote ulimwenguni, haswa zile nchi katika soko ibuka ambazo hupokea pesa nyingi," amesema gavana wa CBK Patrick Njoroge

Chanzo: www.tanzaniaweb.live