Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi za Afrika Mashariki zapumulia mashine madeni ya kimataifa

Debt Nchi za Afrika Mashariki zapumulia mashine madeni ya kimataifa

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi za ukanda wa Mashariki zinatajwa kushindwa kulipa madeni zaidi ya asilimia 30 kutoka kwa wakopeshaji wa kimataifa mara baada ya kusitishwa kwa mpango wa ulipaji madeni uliokuwa ukifanywa na mataifa tajiri zaidi duniani.

Usitishaji huo uliofanywa na mataifa 20 nguli kwa utajiri duniani ya G20

umehamasiha wakopeshaji wa kimataifa kuongeza shinikizo kwa nchi za Afrika kulipa madeni hayo kwa muda uliopangwa.

Hata hivyo inaelezwa kuwa athari za ugonjwa wa Corona zimechangia kuzorota kwa uchumi wa nchi nyingi barani Afrika.

Kulingana na utafiti uliofanywa na kituo cha Jubilee Debt Campaign cha nchini Uingereza umethibitisha kuwa kusitishwa kwa mpango huo kwa nchi masikini kumeongeza shinikizo kwa wakopeshaji wa kimataifa kudai malipo ya madeni hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live