Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi 17 zenye hifadhi kubwa ya Mafuta barani Afrika

Oil Rig And Pumpjack Source Han Maomin Shutterstock Nchi 17 zenye hifadhi kubwa ya Mafuta barani Afrika

Wed, 24 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Libya imefanikiwa kuwa nchi tajiri zaidi kwa mafuta barani Afrika hadi kufikia November 2021, Libya imekusanya mapipa bilioni 48.4 ya akiba iliyothibitishwa. Nigeria inafuatia ikiwa na akiba ya mapipa bilioni 36.9 ya mafuta yasiyosafishwa (crude oil), huku akiba ya Algeria ikijumlisha hadi mapipa bilioni 12.2. Mwaka huu, hifadhi ya jumla ya mafuta ghafi barani Afrika imefikia mapipa bilioni 125.3.

Uzalishaji wa mafuta barani Afrika

Pato la mafuta barani Afrika lilifikia karibu mapipa milioni 8.4 kwa siku hadi mwaka 2019. Ingawa Libya inamiliki hifadhi kubwa zaidi ya mafuta katika bara hilo, imekuwa ikisajili kiwango cha chini cha uzalishaji wa mafuta hivi karibuni, matokeo ya migogoro na hali ya kisiasa isiyo imara imetajwa kuwa chanjo cha kuzorota uzalisha.

Nchi hiyo ilizalisha takriban mapipa milioni 1.1 kwa siku katika mwaka wa 2019. Kwa kulinganisha na Nigeria, nchi inayozalisha mafuta zaidi barani Afrika, ilizalisha mapipa milioni 2.1 kwa siku mwaka huo huo.

Kukuza uchumi

Mnamo mwaka wa 2019, Nigeria iliongoza mauzo ya mafuta ghafi barani Afrika, na zaidi ya mapipa milioni mbili ya mafuta yanauzwa kwenye soko la kimataifa kila siku. Aidha, sekta hiyo ilichangia asilimia saba ya pato la taifa la Nigeria (GDP).

Nchini Angola, ambayo pia ni nchi yenye utajiri wa mafuta, sekta hiyo ilikuwa na mchango mkubwa zaidi katika Pato la Taifa, kwa karibu asilimia 40.

Hapa nimekuweka orodha ya nchi 20 zenye akiba kubwa zaidi ya mafuta barani Afrika.

1 LIBYA 48,363,000,000,

2 NIGERIA 37,070,000,000.

3 ALGERIA 12,200,000,000.

4 ANGOLA 8,423,000,000.

5 SUDAN 5,000,000,000.

6 MISRI 4,400,000,000.

7 CONGO-BRAZZAVILLE 1,600,000,000.

8 UGANDA 2,500,000,000.

9 GABON 2,000,000,000.

10 CHAD 1,500,000,000.

11 EQUATORIAL GUINEA 1,100,000,000.

12 GHANA 660,000,000.

13 TUNISIA 425,000,000.

14 CAMEROON 200,000,000.

15 DR CONGO 180,000,000.

16 NIGER 150,000,000.

17 COTE D'IVOIRE 100,000,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live