Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NSSF Uganda yakusanya trilioni 10.14 kwa mwaka

Pension Payout NSSF Uganda yakusanya mapato mengi 2020/2021

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya mtikisiko wa kiuchumi uliosababishwa na janga la Corona nchini Uganda, inaelezwa kuwa Mfuko wa Hifadhi wa Jamii (NSSF) umepiga hatua kubwa katika makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Taarifa ya fedha nchini humo imeonesha ongezeko la dola bilioni 4.4 kwa mwaka 2020/2021 sawa na shilingi triloni 10.14 za kitanzania kutoka dola bilioni 3.7 kwa mwaka 2019/2020 sawa na shilingi trilioni 8.52 za kitanzania.

Michango ya wanachama imeongezeka hadi kufika dola milioni 385.6 sawa na shilingi bilioni 8.87 za kitanzania kutoka dola 357 sawa na shilingi bilioni 8.22 za kitanzania.

Jumla ya mapato yaliyotokana na uwekezaji hadi mwisho wa mwezi Juni 2021 yalikuwa ni dola milioni 519.8 sawa na shilingi trilioni 1.19 za kitanzania.

Mapato hayo ya uwekzaji mengi yametokana na fedha zilikusanywa kwa ajili ya kupambana na athari za ugonjwa wa Corona kutoka kwa wanachama wa mfuko huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live