Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa kibiashara Kenya na Uganda kuamuliwa Novemba

Kenya Na Ugand Trade Mzozo wa kibiashara Kenya na Uganda kuamuliwa Novemba

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Kenya na Uganda zinatarajia kufanya kikao kitakacho amua hatma ya mzozo wa kibiashara uliopo baina ya nchi hizo mbili ili kuweza kufikia mafanikio ya kudumu ya kiuchumi.

Maafisa kutoka nchini Kenya wanatarajiwa kuwasili nchini Uganda mwezi Novemba kwa ajili ya kujadili muafaka wa uingizwaji wa bidhaa za nchini uganda hasa Maziwa na sukari ambazo zimewekewa kodi kubwa nchini Kenya.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo nchini Kenya, Harry Kimtai, amesema kuwa maafisa hao watakwenda Uganda mwezi Novemba ili kufanya mazungumzo hayo ambayo yalisitishwa kufuatia kuibuka kwa wimbi la tatu la ugonjwa wa Corona.

"Tumesha andika barua kwa mamlaka za Uganda, tumekubaliana kuwa tutakwenda huko mwezi ujao na tutarudi na majibu mazuri" Amesema Katibu huyo.

Wiki iliyopita Serikali ya Uganda ilituma mwaliko kwa mawaziri wa Kilimo na Biashara wa Kenya kwa ajili ya kujadili hatma ya mzozo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live