Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanaridha Kenya avunja rekodi ya dunia 

A35465d313d418ddc436f66bc812d924.jpeg Mwanaridha Kenya avunja rekodi ya dunia 

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MWANARIADHA wa Kenya, Ruth Chepngetich amevunja rekodi ya dunia katika mbio za nusu marathoni, akitumia saa 1:04:02 kwenye Istanbul Half Marathon zilizofanyika Uturuki juzi.

Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 26, mshindi wa mwaka 2017 na 2019, alimwacha mbali Yalemzerf Yehualaw wa Ethiopia katika hatua za mwisho za mbio hizo na kushinda kwa sekunde 38 na kuvunja rekodi ya awali iliyowekwa na Ababel Yeshaneh Ras Al Khaimah wa Urusi Februari mwaka jana.

Yeshaneh aliweka rekodi hiyo katika mashindano ya Ras Al Khaimah Half Marathon aliyotumia muda wa 1:04:31 akivunja rekodi ya raia wa Kenya, Brigid Kosgei aliyetumia muda wa 1:04:49.

Raia huyo wa Kenya anakuwa mwanariadha wa kwanza kutoka nchini humo kuandika rekodi hiyo na kuishangaza dunia kwa uwezo aliouonesha katika mashindano hayo.

Mkenya Hellen Obiri bingwa mara mbili wa dunia wa mbio za mita 5,000 alimaliza wa tatu akitumia saa 1:04:51 mbio za nusu marathoni zenye kasi zaidi katika historia. Ni mara ya kwanza wanawake watatu kumaliza ndani ya dakika 65 katika nusu marathon moja.

Kwa upande wa wanaume, Kibiwott Kandie wa Kenya alishinda kwa kutumia 59:35.

Kandie ambaye aliweka rekodi ya dunia Valencia mwaka jana, aliongoza zikiwa zimesalia dakika 12 na akazuia changamoto ya wenzake wa Kenya Geoffrey Kamworor kudai ushindi kwa sekunde tatu na Roncer Kipkorir akishika nafasi ya tatu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz