Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanariadha wa kenya akutwa amefariki

Mwanariadhya Kenya Mwanariadha wa Kenya, Agnes Tirop

Wed, 13 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanariadha kutoka nchini Kenya, Agnes Tirop(25),amekutwa amekufa ndani ya nyumba yake.

Tirop,aliiwakilisha Kenya katika mashindano ya Olimpiki, yaliyofanyika katika mji wa Tokyo, nchini Japan.

Tirop alishiriki mbio za mita 5,000 katika mbio za wanawake na ameaga dunia Jumatano, Oktoba 13, nyumbani kwake huko Iten, Kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Polisi nchini Kenya, wameliambia Shirika la Habari la BBC kuwa bado uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha kifo chake.

Shirikisho la Riadha nchini Kenya AK, limetuma salamu za rambi rambi kufuatia taarifa za kifo cha mwanariadha huyo ambaye ni mshindi wa medali ya shaba duniani katika mbio za mita 10,000.

"Bado tunafuatilia taarifa zaidi za chanzo cha kifo chake, Kenya imepoteza shujaa, nyota aliyekuwa anakuwa kwa kasi katika ulimwengu wa riadha, tunamshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya"

Mwezi uliopita mwanariadha huyo alivunja rekodi ya wanawake katika mbio za kilomita 10,000 katika mashindano ya Road to Records Race nchini Ujerumani

Alishinda pia mashindano ya nyika ya Afrika mnamo 2014 huko Kampala, Uganda na vile vile Mashindano ya Dunia ya nyika kwa Vijana Duniani mnamo 2013 huko Bydgoszcz, Poland.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live