Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamuziki wa Rwanda Jay Polly afariki dunia akiwa jela

5fd41faf498d4616 Mwanamuziki wa Rwanda Jay Polly afariki dunia akiwa jela

Thu, 2 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mwanamuziki nguli wa Hip hop wa Rwanda Joshua Tuyishime al maarufu Jay Polly, amefariki dunia katika hospitali moja mjini Kigali.

Jay Polly kama anavyofahamika na mashabiki wake alikamatwa mwezi Aprili mwaka huu kwa tuhuma za matumizi ya dawa za kulevyaMashabiki wengi wa muziki nchini Rwanda wameomboleza kifo chake kupitia mitandao ya kijmaii.

Joshua Tuyishime kwa majina kamili alikimbizwa hospitalini kutoka gereza kuu la Kigali baada ya kupatwa na ugonjwa usiojulikana Jumatano usiku.

Kwa mujibu wa taarifa za BBC, Joshua Tuyishime alikimbizwa hospitalini kutoka gereza kuu la Kigali baada ya kupatwa na ugonjwa usiojulikana Jumatano usiku.

Jay Polly mwenye umri wa miaka 33 alikamatwa mwezi Aprili mwaka huu kwa tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya, kesi yake ilikuwa bado inaendelea kortini.

Kulingana na kakake Maurice Uwera, mamlaka ya huduma za magereza nchini humo iliielezea familia kuhusu chanzo cha kifo chake lakini hakupeana maelezo zaidi.

Mashabiki wengi wa muziki nchini Rwanda na wengine kutoka mataifa menginge kijani ambao walimfahamu Jay Polly wamekuwa wakitoa rambi rambi zao kupitia mitandao ya kijamii.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke