Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamuziki Dbanj atangaza hadharani ameoka, aelezea changamoto za maisha

79868bf3e6a46171 Mwanamuziki Dbanj atangaza hadharani ameoka, aelezea changamoto za maisha

Wed, 19 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mwanamuziki kutoka Nigeria Dapo Oyebanjo maarufu Dbanj ametangaza rasmi kwamba ameokoka

- Dbanji aliyasema haya akiwa kwenye tamasha la kikristo mjini Abuja wiki lililopita

- Msanii huyo pia alielezea panda shuka za maisha ambazo amepitia kama msanii lakini alimshukuru Mungu kwa kumwelekeza katika njia za haki

Mwanamuziki maarufu kutoka Nigeria Dapo Oyebanjo almaarufu Dbanji ametangaza kwamba yeye huwa ameokoka na Mungu amemtoa mbali pamoja na familia yake.

Akiwa kwenye tamasha la kikristo mjini Abuja mapema wiki hii, Dbanj alizungumzia safari yake ya wokovu na jinsi amekuwa mtumishi wa Mungu kwa miaka kadhaa.

Dbanj aliendelea kusema kwamba iwapo mashabiki wake huwa makini, wanapaswa kugundua kwamba katika kila albamu yake amekuwa akimpa Mungu sifa na shukrani.

Kulingana na Dbanj, anaposema Mungu ni mshindi huwa anamaanisha na wala sio mzaha.

Mwanamuziki huyo alielezea jinsi maisha yake ya ndoa yamekubwa na changamoto mingi, hata kuna wakati alimpoteza mwanawe wa kwanza lakini miaka mitatu baadaye amejaliwa na watoto wengine wawili.

Mashabiki mitandaoni wamempongeza kwa hatua hiyo, wengi wamemshauri aendelee kushikilia neno la bwana na kuchapa injili kupitia muziki.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

"

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke