Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamuziki Chidinma aendelea kuchapa kazi ya uinjilisti

0fgjhs4ltgcibiq4l Mwanamuziki Chidinma aendelea kuchapa kazi ya uinjilisti

Fri, 14 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mwanamuziki Chidinma Ekile ameasi kufanya miziki za kidunia na sasa ametangaza rasmi kwamba atakuwa akichapa miziki za injili

- Chidinma amevuma kwa nyimba kadhaa ikiwemo Kedike na Yanga na alikuwa kipenzi cha wengi kwa ajili ya kuwa na sauti ya kuvutia

- Kwa ajili ya sauti yake tajika, Chidinma, 30, alikuwa mshindi wa shindano la muziki la Project Fame West Africa mwaka wa 2010

Mwanamuziki maarufu kutoka Nigeria Chidinma Ekile alitangaza hivi maajuzi kwamba ameasi kufanya miziki ya kidunia na atakuwa akiangazia sana miziki za injili.

Kwenye video kadhaa ambazo ameposti kwenye mitandao ya kijamii, Chidinma anaonekana akihubiri injili hata kwa walevi kwenye vilabu.

Mwanamuziki huyo ameingia katika wokovu na kishindo na ana imani kwamba atabadilisha maisha ya wengi.

TUKO.co.ke iliweza kufuatilia kurasa zake za Instagram na imebaini kwamba msanii huyo anatumia mitandao ya kijamii kuhubiri injili na siku ya Jumanne ameitenga kuwa ya kutoa ushuhuda.

Chidinma ametambulika kwa nyimbo kadhaa ikiwemo Kedike na anasemekana alianza kufanya muziki akiwa na umri wa miaka 19.

Kwa ajili ya kuwa sauti tajika, Chidinma, 30, alikuwa mshindi wa shindano la muziki la Project Fame West Africa mwaka wa 2010, hapo ndipo alipopata umaarufu zaidi katika ulingo wa muziki.

Msanii huyo alitangaza kwamba atakuwa akifanya muziki wa injili pindi alipotimia umri wa miaka 30, habari ambazo zilipokelewa na hisia tofauti miongoni mwa mashabiki wake.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zai hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke