Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke aliyezaa na Eric Omondi alalamika kukosa matunzo ya mtoto

Cb2ae9f3b06779d5 Mwanamke aliyezaa na Eric Omondi alalamika kukosa matunzo ya mtoto

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Aliyekuwa mwanahabari wa runinga ya Citizen Jacque Maribe alimefichua kwamba amekuwa akimfunika mchekeshaji Eric Omondi kwa miaka saba kwa kutowajibikia mtoto wao.

Mama huyo wa mtoto mmoja alifichua kwamba amekuwa akidanganya kwamba Omondi humtunza mtoto wao akiwa na lengo la kutompaka tope mchekeshaji huyo.

Mchekeshaji Eric Omondi na aliyekuwa mwanahabari wa runinga ya Citizen Jacque Maribe wana mtoto pamoja kwa jina Zahari. Maribe amemkashifu hivi maajuzi Omondi kwa kutowajibikia mtoto wao

Kupitia kwenye mtandao wa Instagram, Maribe pamoja na dadake Cate Maribe walimkashifu Omondi kwa kumtelekeza mtoto wake.

Akizungumza na bloga Eve Mungai, alisema amekuwa akidanganya kwamba Omondi hujitwika majukumu ya mwanawe akiwa na lengo la kutomchafulia jina.

Akimjibu Maribe, Omondi alikuwa na haya ya kusema, " Ni mahojiano mangapi umefanyiwa ukikiri kwamba mimi ni baba muwajibika, mwenye upendo na mimi hukuwepo kila mara mtoto wangu anaponihitaji," Aliuza Eric.

Maribe naye alikuwa na haya ya kumjibu," Niliamua kukufunika kwa sababa nilikuwa namlinda mtoto wangu hata na wewe mwenyewe, naona mitandaoni unajifanya kuwa mtu tofauti lakini kwa ukweli hauko," Maribe aliongezea.

Aidha, Maribe ametishia kumshtaki Omondi kuhusu malezi ya mtoto wake.

Imeripotiwa kwamba sarakasi kati ya Eric na Jacque ilianza baada ya msanii huyo kupakia mitandaoni picha ya mwanamuziki Missp akidai kwamba ana ujauzito wake.

" Nilikutana na huyu msichana miezi tano iliyopita kwenye tamasha moja nililokuwa nawakilisha, chenye kilitokea kati yangu na yeye kilishatendeka na namhuahidi kwa mba nitakuwa baba wa kuwajibika kwa mtoto wetu.Watoto ni baraka kutoka kwa Mungu," Omondi aliandika Instagram.

Mashabiki wake walimpongeza kwa hatua hiyo huku wengine wao wakisema ni baadhi ya picha kutoka kwenye wimbo ambao Missp anatarajia kuutoa.

Maribe pia alitoa kauli yake akiashiria kwamba Omondi hawezi kuwa baba mwajibikaji;" Kuwajibika? @catewamaribeMaribe, kuja hapa mimi siwezi nikazungumza, miaka saba ya kuwajibika? Aliandika kikejeli.

Hata hivyo,Maribe alisema hajutii kumlea mtoto wake bila ya usaidizi wa babake kwa sababu alishazoea.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke