Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanahabari nyota Alex Mwakideu aomba msaada wa KSh 900,000

F8d2029361c92dc7 Mtangazaji Alex Mwakideu

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mtangazaji maarufu Alex Mwakideu amewaomba wahisani wajitokeze ili wachangishe fedha zitakazo gharamia matibabu ya dadake hospitalini ambaye yuko katika chumba cha ICU.

Mwakideu alisema dadake Rozina Mwakideu alipatikana na virusi vya COVID -19 mwezi mmoja uliopita na gharama ya matibabu imekuwa ghali mno.

" Dadangu Rozina Mwakideu amekuwa hospitalini kwa zaidi ta mwezi mmoja, kusema ukweli, gharama ya kutibu ugonjwa wa COVID-19 ni ghali sana, Rozina amekuwa katika chumba cha ICU kwa wiki mbili na kwa sasa anaendelea kupata nafuu. Madaktari wametushauri tumruhusu aende nyumbani lakini hatuna fedha zozote za kulipa bili yake Kwa sababu wagonjwa wanaoendelea kupona, kutengwa hospitalini ni hatari hasa kwa wale ambao wameambukizwa tayari," Alisema Mwakideu.

" Tunajaribu kuchanga KSh 900,000 ili tuweze kulipa bili hiyo, tununue mashine ya kumpa Oksijeni na matibabu mengine anayohitaji. Tunaomba msaada wa kifedha tafadhali pamoja na maombi," Aliongezea Mwakideo.

Rozina ni mke wa zamani wa mhubiri na mwandishi wa vitabu Robert Burale, walijaliwa mtoto mmoja wa kike walipokuwa katika ndoa.

Inasemekana kwamba wawili hao walioana kwa muda wa mwaka mmoja pekee na wakaachana kwa madai kwamba Burale alikuwa anamficha mkewe mambo mengi ambao hayapaswi kuwekwa siri katika ndoa.

Rozina aliongezea kwamba ingawa wote wawili walikuwa wameokoka, lakini kuna mambo kadhaa ambayo hangestahimili katika ndoa.

Aidha, wasanii mbali mbali wameahidi kusimama na Mwakideu

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke