Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa mbunge ajiua kwa risasi

Sankok .jpeg Sankok na familia yake

Tue, 3 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa kiume wa Mbunge Sankok nchini Kenya ameipiga risasi na kujiua nyumbani kwao. Memusi Sankok, mwenye umri wa miaka 15, inadaiwa alijifyatulia risasi kwa kutumia bastola ya baba yake mzazi jana, Jumatatu, majira ya mchana.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kuhusu tukio hilo, inasemekana aliichukua bastola hiyo, iliyokuwa imefichwa kwenye sanduku salama, kwenye bafu ya baba yake.

Kijana huyo alikuwa mwananfunzi wa kidato cha nne, katika Shule ya Sekondari ya Kericho. Haijabainika mpaka sasa sababu ya Memusi kuamua kujitoa uhai, huku uchunguzi wa mkasa huo ukiendelea.

Bastola hiyo iliyokuwa ikitumika na Mbunge huyo na kusababisha mauaji ya mwanawe, tayari imetwaliwa na maofisa wa polisi wa Idara ya Ujasusi wa Jinai (DCI) ili ikaguliwe.

Akithibitisha kisa hicho, Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Narok Kusini (DCC), Felix Kisalu alisema maofisa wa DCI wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: