Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Salah homa ya jiji la Nairobi

Salahhhh Mo Salah homa ya jiji la Nairobi

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: eatv.tv

Mshambuliaji nyota wa Liverpool Mohamed Salah ni moja ya wachezaji wa Misri waliotua nchini Kenya, wakiwa na timu ya taifa ya nchi hiyo mahususi kwa mchezo wa kufuzu michuano ya AFCON inayotarajiwa kuchezwa kesho tarehe 25/03/2021.

Submitted by Tigana Lukinja on Jumatano , 24th Mar , 2021 Mo Salah akishangilia moja ya magoli aliyofunga

Mo Salah ni miongoni mwa wachezaji bora wa Kiafrica wanaopeperusha vyema bendera Ulaya, akishiriki kwenye mafanikio mabalimbali ndani ya kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza na mabingwa wa kombe la dunia kwa ngazi ya vilabu pamoja na mabingwa wa Ulaya kwa msimu wa 2018/2019 klabu ya Liverpool.

Kupitia mafanikio yake ya sasa Mo Salah amekuwa gumzo katika kila kona ya Nairobi na Kenya kiujumla kwa wadau wa mchezo wa soka, mjadala mkubwa pia ukiwa nani atamkaba mchezaji huyu kutokana na kukosekana kwa mlinzi wao Joash Onyango wa klabu ya Simba aliyeumia akitumikia timu yake kwenye mchezo dhidi ya El Merrikh.

Takwimu za Mo Salah katika msimu huu ndani ya kikosi cha Liverpool amefunga magoli 25 katika michezo 39 hadi sasa, ataongoza mashambulizi ya timu yake ya Taifa ikiwa ni mechi ya kundi G lenye mataifa ya Kenya, Togo pamoja Comoro.

Chanzo: eatv.tv