Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mo Salah Awasili Kenya Kukipiga na Harambee Stars

Salah?fit=624%2C416&ssl=1 Mo Salah Awasili Kenya Kukipiga na Harambee Stars

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mo Salah Awasili Kenya Kukipiga na Harambee Stars March 25, 2021 by Global Publishers



KIKOSI cha Misri wakiwa na staa wao Mo Salah wamewasili jijini Nairobi Jumanne kwa ajili ya mchezo kati ya Mafarao hao na Harambee Stars, mchezo utakaopigwa katika uwanja wa michezo wa kimataifa, Kasarani leo Alhamisi, Machi 25, 2021.

Ushindi wa Misri utawahakikishia wanafuzu katika kinyang’anyiro hicho cha Afrika kitachofanyika nchini Cameroon mwaka ujao. Kenya pia inauhitaji sana ushindi huu ili kujiongezea nafasi ya kufuzu.

Katika hatua nyingine, Mo Salah ameripotiwa na gazeti la Independent la Misri kuwa ameomba kujitenga na wenzake, lakini haijafahamika kama ombi lake limetekelezwa. Uamuzi wa Salah wa kuishi tofauti na wenzake unaaminika kuwa jitihada za kujitenga.

Salah alikutwa na virusi vya Covi-19 wakati wa safari ya hivi karibuni barani Afrika kwa ajili ya majukumu yake ya kimichezo mwaka jana, pia mchezaji mwenzake Mohamed Elneny, anayekipiga katika klabu ya Arsenal. Elneny pia yuko kwenye kikosi kitakachopepetana na Kenya.

Chanzo: globalpublishers.co.tz