Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlipuko wa Lori la Mafuta waua atu 90 Nigeria

Lori La Mafuta Nigeria Mlipuko wa Loro la Mafuta waua atu 90 Nigeria

Thu, 17 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 90 wameuawa na karibu 50 kujeruhiwa katika Mlipuko wa Lori la Mafuta katika Jimbo la Jigawa, Kaskazini Magharibi mwa Nigeria, kulingana na polisi wa eneo hilo.

Lori la Mafuta lilipinduka katika Mji wa Taura na wakazi walikimbilia eneo la tukio ili kupata mafuta yaliyokuwa yakivuja.

Lori hilo lilikuwa likisafiri kutoka Kano kuelekea mjini Nguru, Jimbo la Yobe.

“Takriban watu 94 walikufa. Walichomwa kiasi cha kutotambulika na wengine 50 walihamishwa kwa matibabu katika hospitali ya mji wa Ringim,” msemaji wa polisi wa jimbo hilo alisema kutoka Jigawa.

Milipuko ya Lori la Tanki ni ya kawaida nchini Nigeria. Mwezi uliopita, watu 59 walipoteza maisha katika Jimbo la Niger baada ya lori kugongana na Lori lililokuwa limebeba abiria na mifugo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live