Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkenya ajitokeza akidai msanii Ali Kiba ni baba yake

59ad49a690d4e250 Mkenya ajitokeza akidai msanii Ali Kiba ni baba yake

Thu, 23 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mwanamuziki chipukizi kutoka Kasarani anaamini kuwa Ali Kiba ni baba yake mzazi na anataka kukutana nayeKulingana na Bigpoint almaarufu Ali Kiba Junior, mama yake ndiye alimwambia nyota huyo ni baba yakeHata hivyo, Bigpoint alisema mama yake alimkimbia na hajui mahali alikoMwanamuziki Mkenya chipukizi anaamini kuwa Ali Kiba ni baba yake mzazi.

Bigpoint, ambaye jina lake la kisanii ni Ali Kiba Junior, alisema mama yake alimwambia Mkurugenzi Mkuu wa Kings Music ni baba yake.

Kulingana na kijana huyo kutoka Mwiki, Kasarani, huguzwa sana akisikiza nyimbo za Kiba.

“Mama yangu alikuwa akiniambia Ali Kiba ni babu yangu tangu nikiwa mtoto. Kwa hivyo kila mara ninaposikiza wimbo wake, kuna kitu cha kipekee ambacho mimi huhisi ndani yangu.

"Natumania kuuayan naye ioli niweze kuhakikisha kuwa ni baba yangu," alisema.

Mama amtupaBigpoint, ambaye alizaliwa Mombasa lakini kukulia Limuru na Bomet, alisema yake alimfahamisha kumhusu Kiba wakati alikuwa katika shule ya msingi.

Hata hivyo, Bigpoint alisema mama yake alimkimbia na hajui mahali aliko baada ya kumuwacha Bomet na baba yake wa kambo.

“Sina habari mahali mama yangu aliko, alituwacha. Aliondoka tu na sijawahi kumuona,” alisema.

Usuli wa Kiba

Bigpoint anaamini kuwa Kiba ni baba yake mzazi kwani ni yeye tu ndiye mwanamziki katika familia yao.

“Simfahamu mtu mwingine katika familia yangu ambaye ni msanii. Kwa hivyo nimerithi talanta ya Kiba,” alisema.

Bigpoint alisema iwapo atakutana na Kiba, angleipenda muimbaji huyo Mtanzania kupiga jeki taaluma yake na kuthibitisha endapo ni mzazi wake.

“Ningependa kukutana na wewe baba. Hiyo ni ndota yangu,” aliambia White Media.

Msanii huyo alipata umaarufu baada ya kutembea na bango lililosoma: “Hamjambo Wakenya, jina langu ni Bigpoint, na ninamtafuta baba yangu kwa jina Ali Kiba.”

Maoni ya wanamtandao@_mzae_254: “Kwa hivyo anamafuta Ali Kiba jijini Nairobi.”

@nairobikulture: “Tunataka DNA tifanywe”

@glockboymalcolm: “Kweli mwafanana”

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke