Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miquissone rasmi Al Ahly

MIQUISSONE MISRI Luis Miquissine akitambulishwa rasmi Al Ahly

Fri, 27 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Al Ahly imetangaza rasmi kukamilisha usajili winga wa kimataifa wa Msumbiji Luis Miquissone (26) kutoka klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka minne.

Miquissine amefanya vizuri na klabu ya Simba na ni mmoja kati ya wachezaji ambao waliwapa shida sana Al-Ahly katika mechi za Ligi ya Mabingwa barani Afrika walipokutana msimu uliopita. Ikiwemo kuwafunga goli la pekee katika Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Taarifa zinasema kwa mwaka nyota huyo atapokea mshahara wa bilioni 1 na milioni 150 kwa mwaka ikiwa ni sawa na milioni 95 kwa mwezi.

Miquissone alijiunga na Simba SC akitokea klabu ya UD Songo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live