Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya Stars na Kenya yafutwa

11389 JPM+PIC Mechi ya Stars na Kenya yafutwa

Fri, 19 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MECHI ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' na Kenya 'Harambe Stars' iliyopangwa kuchezwa leo kwenye uwanja wa Nyayo jijini Nairobi kuanzia saa 9:00 alasiri imefutwa.

Sababu kuu ya kufutwa kwa mechi hiyo ni kutokana na msiba mkubwa uliopo nchini Tanzania baada ya jana Jumatano kufariki kwa Rais wa nchi Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa amelazwa kwenye hosptali ya Mzena jijini Dar es Salaam akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Taarifa rasmi kutoka kwenye Shirikisho la Soka Tanzania 'TFF' imeeleza kuwa licha ya kuahirishwa kwa mechi hiyo lakini kikosi cha Stars kitasalia nchini Kenya kikijifua kwa maandalizi ya mechi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwakani (Afcon 2020).

Rais Magufuli atakumbukwa kwa kuwa moja ya nguzo na mhimili mkuu katika soka la Tanzania hususasani timu za taifa kwa kuzisaidia kimawazo, kiuchumi na hata kiuongozi wakati akiwa madarakani.

Ndani ya miaka sita ya utawala wa Magufuli Taifa Stars imeweza kupata mafanikio mbali mbali na kubwa zaidi ikiwa ni kufuzu Afcon mwaka 2019  tangu mwaka 1980 timu hiyo ilivyofanya hivyo kwa mara ya kwanza.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz