Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchekeshaji wa Churchil Show, MC Jessy kuwania ubunge 2022

B690fedbe1008b29 Mchekeshaji wa Churchil Show, MC Jessy kuwania ubunge 2022

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

MC Jessey anatazamia kumpokonya kiti mbunge wa sasa wa Imenti Kusini, Kathuri Murungi, ambaye yuko katika muhula wake wa piliMsanii huyo alitawazwa rasmi na wazee wa eneo bunge hilo mnamo Jumamosi, Novemba 6Jessey anajiunga na mchekeshaji Jalang'o ambaye pia ametangaza azma yake ya kuwania kiti cha ubunge mwakaniMvunja mbavu maarufu wa Churchill Show, MC Jessy amejitosa rasmi katika siasa akitazamia kuwania kiti cha ubunge cha Imenti Kusini katika Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Msanii huyo alithibitisha azma hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kutawazwa rasmi na wazee wa eneo bunge hilo mnamo Jumamosi, Novemba 6.

"Wikendi, nilishukuru wazee walionilea waliponiidhinisha na kunipa baraka na majukumu ya kuongoza eneo bunge la Imenti Kusini kama Mbunge," aliandika.

"Jamii yetu lazima ijiweke sawa kwa Wazee kutowaogopa Vijana au kuhisi kutengwa nao. Vazi limepitishwa na kila kizazi lazima kililinde na kulieneza zaidi," aliongeza.

MC Jessy alipakia picha za hafla hiyo kwenye ukurasa wake akionyeshwa akivishwa mavazi ya kitamaduni ya kiongozi wa jamii hiyo.

MC Jessey anatazamia kumpokonya kiti mbunge wa sasa wa Imenti Kusini, Kathuri Murungi, ambaye yuko katika muhula wake wa pili.

Jessey anajiunga na mchekeshaji Jalang'o ambaye pia ametangaza azma yake ya kuwania kiti cha ubunge mwakani.

Jalang'oKwingineko, mtangazaji na mchekeshaji maarufu Felix Odiour almaarufu Jalang'o ambaye pia anaazimia kuwa mbunge wa Lang'ata baada ya uchaguzi mkuu wa 2022 amewarai wafuasi wake waache kumuitwa 'Mheshimiwa'.

Kulingana na Jalang'o, anataka achaguliwe na wakazi, aingie bungeni, awahudumie ipasavyo ndiposa aitwe mheshimiwa.

"Wanasema ati Jalang'o anaongea tu sai kwa sababu hajaingia bunge, tunajua akiingia atatusahau lakini nataka kuwahakikishia kwamba kauli mbiu yangu ni 'Utu na Watu' kwa hivyo msiniite mheshimiwa kama sijaingia ofisini," alisisitiza Jalas.

Jalang'o ambaye atawania kiti hicho kwa tiketi ya chama cha ODM, alisema atahakikisha kwamba anatimiza matwakwa ya wakazi wa Lang'ata na kufanya maendeleo makubwa.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke