Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchekeshaji Anne Kansiime aomboleza kufuatia kifo cha mamake

Eb1af847f0b89708 Mchekeshaji Anne Kansiime aomboleza kufuatia kifo cha mamake

Sun, 6 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mchekesha maarufu kutoka Uganda Anne Kansiime anaomboleza kufutia kifo cha mamake kilichotokea Jumapili, Juni 6.

Kansiime alitangaza habari za kifo cha mamake kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

"Kwa kweli njia za Mungu ni za ajabu, sio kama za binadamu, Mama leo ametuacha, ameaga dunia," Aliandika Kansiime.

Mashabiki wake wamemtumia jumbe za pole anapopitia wakati huu wa huzuni na majonzi.

Kifo cha mamake kinajiri takribani miezi miwili baada ya mchekeshaji huyo na mumewe Skylanta kujaliwa mtoto wao wa kwanza.

Wawili hao walianza kuchumbiana mnamo 2018 hii ni baada ya Kansiime kuachana na mumewe wa zamani, Gerald Ojuok, mnamo 2017.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke