Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa wa Kenya wanao ingiza pesa nyingi kwa video za TikTok

Tiktok.jpeg Mastaa wa Kenya wanao ingiza pesa nyingi kwa video za TikTok

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wengine wakiutumia mtandao wa Tik Tok kama sehemu ya burudani, wapo wanaoutumia mtandao huu kama moja ya nyaja za kuwaingizia kipato .

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Habari la Forbes katika chapisho la mwaka 2020, ilionesha kwa uwazi kiasi ambacho baadhi ya watumiaji wa mtandao huo wanaingiza duniani kote.

Ripoti hiyo iliwataja nyota 7 wa nchini Kenya wanaopiga mpunga mrefu kutoka na video wanazoweka katika mtandao huo.

Moja kati ya hao ni kijana Addison Rae wa miaka 19 , yeye amejipatia kiasi cha dola milioni 5 ambayo ni sawa na bilioni 11.6 za kitanzania kwa mwaka 2019.

Msanii Azziad Nasenya wa miaka 21, yeye amejiapatia umarufu mkubwa kupitia video zake anazoweka katika mtandao huo, anakadiriwa kuwa na wafuasi zaidi ya milioni 1.

Azziad anaingizia kiasi cha Sh.500,000 za Kenya sawa na Milioni 10.5 za Tanzania, umaarufu wake umemsaidia pia kujitengenezea kipato binafsi kwa kufungua chaneli katika mtandao wa YouTube ambapo staa huyo anaendesha biashara yake ya kuuza viatu.

Mwingine ni Ajib Gathon, yeye alianza kutumia mtandao huu, mara baada ya ugonjwa wa Corona kuibuka na kupelekea vyuo kufungwa, aliichukia hali ya upweke wa kukaa tu ndani, ndipo aliona arekodi video akiwa anacheza, video zake zilipendwa sana, ghafla akapata wafuasi wengi na kumuwezesha kupata kiasi cha Shilingi laki 4 za Kenya, ambazo ni sawa na Shilingi milioni 8.40 za Tanzania.

Alma Mutheu wa miaka 23, yeye anaingiza kiasi cha Shilingi elfu 30 za Kenya sawa na Shilingilaki 630,000 za Tanzania.

Mtandao huu, ulianzishwa mwaka 2018, wakati ambao hakuna aliyedhani kuwa kuna siku utaweza kubadilisha maisha ya watu kwa kuwaongezea kipato.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live