Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamlaka za usafiri wa anga Afrika zapoteza trilioni 23.19 kwa Corona

Anga Usafiri Mamlaka za usafiri wa anga Afrika zapoteza trilioni 23.19 kwa Corona

Sun, 26 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashirika ya ndege barani Afrika yanatajwa kupoteza dola bilioni 10 sawa na shilingi trilioni 23.19 za kitanzania kwa mwaka 2020 kufuatia kuibuka kwa ugonjwa wa Corona barani humu.

Upotevu huu umesababishwa na vizuizi vya kusafiri vilivyowekwa katika Mamlaka za usafiri wa anga duniani kote hali iliyopolekea watu wengi kusitisha safari zao.

Sekta ya utalii inatajwa kuwa kinii cha kushuka kwa mapato hayo ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Umoja wa nchi za Afrika Mashariki, imeonesha kuwa takribani dola bilioni 4.8 sawa shilingi trilioni 9.27 za Tanzania zimepotea kutokana na watalii kupungua katika kipindi cha mwaka 2020.

Taarifa hii ya upotevu wa mapato katika sekta hii imetolewa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EABC ya nchini Rwanda, John Bosco Kalisa, katika mkutano wa wadau wa sekta binafsi nchi humo.

Mkurugenzi huyo amezishauri Mamlaka za usafiri wa anga zipunguze ada pamoja na ushuru kwa watu wanaotumia usafiri huo katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live