Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamelodi yaipiga Belouzidad mkono

A65be21d0d4a8d972b51dad22d34f9fb Mamelodi yaipiga Belouzidad mkono

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya wenyeji wao CR Belouzidad ya Libya katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam jana.

Katika mchezo huu ambao Mamelodi walitawala kwa dakika zote 90, ilishuhudiwa mshambuliaji wa timu hiyo, Thenba Zwane akiibuka nyota wa mchezo huo baada ya kufunga mabao mawili, huku Shalulile Maboe na Roméo wakiifungia timu hiyo mabao mengine.

Licha ya CR Belouzidad mchezaji wao mmoja kutolewa nje kwa kadi nyekundu mwanzoni mwa kipindi cha kwanza, lakini kilichowaponza wenyeji hao wa mchezo huo ni kutaka kuwashambulia wapinzani wao Sundowns ilhali wapo pungufu.

Kwa ushindi huo, Mamelodi Sundowns imefikisha pointi sita na kukaa kileleni mwa kundi B, ikifuatiwa na TP Mazembe iliyo na pointi, mbili huku CR Belouzidad ikishika nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi moja sawa na Al Hilal ya Sudan.

Mechi hiyo imechezwa Dar es Salaam baada ya CR Belouzidad kuomba kutumia uwanja wa Mkapa kama uwanja wake wa nyumbani kwenye michuano hiyo kutokana na tishio la virusi vya corona nchini kwao.

Chanzo: habarileo.co.tz