Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makumi ya watu wakamatwa katika maandamano ya kupinga serikali ya Uganda

Makumi Ya Watu Wakamatwa Katika Maandamano Ya Kupinga Serikali Ya Uganda.png Makumi ya watu wakamatwa katika maandamano ya kupinga serikali ya Uganda

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Makumi ya watu wamezuiliwa katika mji mkuu wa Uganda Kampala baada ya kujiunga na maandamano yaliyotawanyika ya kupinga ufisadi kupinga marufuku rasmi.

Mawakili walisema takriban watu 60, akiwemo mtangazaji mashuhuri wa TV na viongozi watatu vijana wa maandamano, walifikishwa mahakamani kwa haraka na kurudishwa rumande kwa kushiriki maandamano ya kuelekea bunge la nchi hiyo siku ya Jumanne.

Rais Yoweri Museven, ambaye ameitawala Uganda kwa takriban miongo minne, alikuwa ameonya kabla ya tukio kwamba waandamanaji "wanacheza na moto".

Maandamano hayo yaliandaliwa kwenye mitandao ya kijamii huku kukiwa na hasira kutokana na madai ya muda mrefu ya ufisadi yanayowahusisha maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa umma.

Maandamano hayo yalichochewa kwa kiasi kikubwa na maandamano ya mwezi uliopita katika nchi jirani ya Kenya kwa sehemu ambayo yalimlazimisha Rais William Ruto kusitisha nyongeza ya kodi iliyopangwa.

Hapo awali polisi walitangaza kuwa walikataa kutoa kibali cha kuandamana na hawataruhusu maandamano yoyote ambayo yanatishia "amani na usalama" wa Uganda.

Chanzo: Bbc