Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majibu ya Uchunguzi: Agnes Tirop alidungwa kisu na kupigwa kichwani

3dd76542b1446725 Majibu ya Uchunguzi: Agnes Tirop alidungwa kisu na kupigwa kichwani

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Upasuaji wa maiti uliofanywa Jumanne, Octoba 19, ulionyesha kuwa Agnes Tirop alifariki kutokana na majeraha ya kudungwa kisu na kupigwa na kifaa butu.

Wanapatholojia wawili kutoka hifadhi ya hospitali ya Rufaa ya Iten walifanya upasuaji wa maiti Wazazi wa marehemu Vincent na Diana Tirop walikuwepo. Upasuaji wa maiti uliofanyiwa mwili wa mwanariadha Agnes Tirop, 25, ulionyesha kuwa alifariki kutokana na majeraha ya kudungwa kisu shingoni na kupigwa na kifaa butu kichwani.

Mwili wa mkimbiaji huyo ulipatikana ukiwa umelowa damu Jumatano, Oktoba 13, na majeraha ya kisu na kudaiwa kutekelezwa na na mpenzi wake Ibrahim Rotich.

Wanapatholojia wawili kutoka hifadhi ya Hospitali ya Rufaa ya Iten waliofanya upasuaji huo wa maiti walisema pia alipigwa na kifaa butu.

"Tumefanya upasuaji huu kama timu ya wanapatholojia na watalaam wa uchunguzi kutoka ICRH," alisema mwanapatholojia wa serikali Dorothy Njeru ambaye aliongoza zoezi hilo.

"Uchunguzi umeonyesha majeraha kwa sababu ya kupigwa. Majeraha ya visu yalikuwa shingoni na jeraha ya kifaa butu lilikuwa kichwani," akaongeza.

Mshukiwa mkuu akamatwaMshukiwa mkuu katika mauaji hayo, Rotich alikamatwa siku moja baada ya kisa hicho akijaribu kutoroka mkono wa sheria na kuzuiliwa kwa siku 20.

Rotich alifikishwa mbele ya hakimu Charles Kutwa mnamo Jumatatu, Oktoba 18, ambapo upande wa mashtaka uliomba azuiliwe kwa siku 20 zaidi.

Korti iliagiza kuwa azuiliwe katika Kituo cha Polisi ca Railways mjini Eldoret akisubiri kufanyiwa uchunguzi wa akili katika Hospitali ya mafunzo na Rufaa ya Eldoret.

Kesi hiyo itatajwa Novemba 9.

MazishiWakati huo huo mipango ya mazishi ya Tirop yanaendelea nyumbani kwao katika kaunti ya Nandi

Mazishi hayo yanatarajiwa kufanyika Jumamosi, Oktoba 23, siku ambayo anglitimia umri wa miaka 26.

Jumatatu, baba yake alisema Rotich hakufuata taratibu ipasavyo za kumuoa binti yake na familia hivyo yake haitakani kuhudhuria mazishi yake.

"Sikuwa nimempean kwa ndoa; sijui hata familia ya mtu huyo. Hawakuwahi, hata mara moja kuja kwenye kiwanja changu na sasa hawapaswi pia kuja kwa mazishi yake," baba huyo aliye na huzuni alisema.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke