Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Mahakama yamfungia Mwanasiasa kugombea urais Rwanda

Bernard Ntaganda Bernard Ntaganda

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu nchini Rwanda imemfungia Mwanasiasa wa Upinzani Bernard Ntaganda kugombea Urais katika uchaguzi wa Julai 15,2024.

Katika uamuzi wake Mahakama hiyo ilisema Mwanasiasa huyo na Mwanzilishi wa Chama cha PS-Imberakuri, alipoteza haki ya kisiasa aliposhtakiwa mwaka wa 2011 kwa kuhatarisha usalama wa taifa kwa kuunga mkono ukabila na kuitisha maadamano haramu.

Mwezi Machi Mwanasiasa mwingine wa Chama cha Upinzani cha DALFA Umulinzi,mwanamama,Victoire Ingabire alifungiwa kugombea ingawaje alikata rufaa katika Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Bw.Beranrd Ntaganda amefahamisha kuwa anaweza kukata rufaa katika mahakama ya EAC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live