Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maguri kuweka rekodi Zimbabwe

Zimbabwe 111 Maguri kuweka rekodi Zimbabwe

Tue, 23 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

STRAIKA Elias Maguri  anayekipiga katika klabu ya FC platinum yupo mbioni kutengeneza rekodi ya kucheza timu moja kwa misimu miwili mfululizo.

Maguri tangu aanze kucheza soka lake hajawahi kudumu katika timu kwa misimu miwili kutokana anapokuwa katika majukumu yake msimu unaofata hupandiwa dau na timu nyingine.

Mshambuliaji huyo aliliambia Mwanaspoti yupo katika hatua za mwisho kumalizana na mabosi wa klabu hiyo kwa lengo la kuendelea kusalia mpaka msimu ujao.

"Itakuwa ndio timu yangu kucheza misimu miwili, mpaka sasa tunaenda vizuri kuna baadhi ya vipengele kwenye mkataba tunaviweka sawa".

"Nazani hapa naweza kukaa maana tunaelewana , labda ligi isiwe ndani ya wakati ndio naweza kuomba kuondoka" alisema mshambuliaji huyo.

Maguri alisema sababu kubwa ambayo inamfanya asiwe anadumu katika timu ni kutokana na huwa hapendi magumashi lakini pia anaangalia zaidi maslahi yake.

"Mara nyingi mkataba wangu ni mwaka mmoja, sasa kama kwenye Ligi umekiwasha  na uko na mkataba mfupi huwezi kushindwa kuondoka, hiyo ndio sababu kubwa".

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz