Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maandamano Uganda: Usalama waimarishwa

Maandamano Uganda: Usalama Waimarishwa Huku Vijana Wakijiandaa Kuandamana .png Maandamano Uganda: Usalama waimarishwa huku vijana wakijiandaa kuandamana

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Hali ya usalama imeimarishwa mjini Kampala Uganda huku wanajeshi wenye silaha wakionekana kuizingira mitaa baada ya vijana kupanga kuandamana hadi kwenye bunge kuwasilisha madai yao, ikiwa ni pamoja na kujiuzuru kwa Spika.

Awali rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni aliwaonyea waandamanaji kwamba "watakuwa wakicheza na moto" ikiwa wataendelea na mipango ya kuandaa maandamano ya kupinga ufisadi hadi bungeni siku ya Jumanne.

Haya ni baadhi ya madai ya waandamanaji waliyopanga kuyawasilisha bungeni leo:

Mbunge yoyote aliyehusika na kashfa yoyote ya ufisadi lazima ajiuzuru wakati uchunguzi ukiendelea.

Kufanyika kwa ukaguzi wa mali na mtindo wa maisha wa wabunge na kuutangazwa Kukatwa kwa mishahara na marupurupu ya wabunge wote hadi shilingi milioni 3 za Uganda.

Kuwaruhusu Waganda kuendelea kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kukusanyinyika kwa amani bila kizuizi.

Chanzo: Bbc