Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MTN yatoa hisa za bure kwa wawekezaji Afrika Mashariki

Mtn Wawekezaji Afrika Mashariki wapatiwa hisa za bure na MTN

Tue, 12 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawekezaji wa Afrika Mashariki wamepewa hisa za bure ili kuwahamasisha kununua hisa katika kampuni ya mawasiliano ya MTN Uganda ambayo imetangaza ofa ya dola milioni 250 sawa na Bilioni 576.750 za kitanzania iliyopewa jina la 'initial public offering' IPO.

Kampuni hiyo kutoka nchini Afrika Kusini inauza hisa zake zaidi ya bilioni 4.47 katika soko kuu la hisa nchini humo, ambapo hisa moja inauzwa kwa shilingi 128 za kitanzania.

Katika kufanikisha ofa hiyo ambayo imelega kuuza walau hisa bilioni 1.1, MTN imetoa nafasi hiyo kwa wawekazaji wanaotarajiwa kushiriki katika ofa hiyo kupatiwa hisa za bure katika vitengo 5 hadi 10 kati ya vitengo 100 vilivyotengwa katika mchakato huo.

"Waombaji wanaostahili kwa maana ya waliokidhi viwango atapokea mgao huu wa hisa za bure, zipo hisa ambazo watalazimika kununua na ieleweke kuwa hii ni seheu ya motisha kwa washiriki wote wa ofa hii" imesema taarifa ya MTN.

Pia imesisitia kuwa hakuna upendeleo wa aina yoyote , isipokuwa kwa washiriki wazawa wao watapatiwa nafasi zaidi ya kushiriki katika ofa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live