Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MTC wanukia robo fainali wavu Tunisia

WhatsApp Image 2021 04 20 At 8.30.31 AM.jpeg MTC wanukia robo fainali wavu Tunisia

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: eatv.tv

Wawakilishi wa nchi katika michuano ya Wavu klabu bingwa Africa MTC kutoka Mwanza ,wapo katika hatua nzuri kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kufanikiwa kushinda seti 3-1 dhidi ya Wolaita Dicha ya Ethiopia

Submitted by Tigana Lukinja on Jumanne , 20th Apr , 2021 kikosi cha MTC kinachopeperusha bendera vyema Tunisia

Ushindi unaowafanya kuwa na alama 4 baada ya mchezo wa kwanza kupata alama moja inayotokana na kupata seti 2 katika mchezo wa kwanza licha ya kupoteza kwa seti 3-2

Majaliwa yawa MTC yapo katika mchezo wa leo kwenye dhidi ya wenyeji Olymipic Kalebia wanaoongoza kundi hilo ambapo itatoa hatma japo mazingira yake si mabaya kwa kuwa wanahitajika hata kama watapotez a basi wapate angalao seti 2 ili waweze kupata alama 1 itakayowafanya kufuzu



Michuano hiyo iliyoanza tarehe 18-4-2021 inatarajiwa kumalizika 28-4-2021 inashirikisha timu ishirini zilizopo kwenye makundi, inaonekana kufanikiwa sana kutokana na ushindani uliopo

Licha ya MTC kufanya vyema hadi sasa lakini mafanikio mengine kwa Watanzania yapo kwa mwamuzi wa kimataifa anayechezesha michuano hiyo Alfred Selengia ambaye alichezesha vizuri mechi KPA ya Kenya na APR ya Rwanda

Hadi sasa msimamo wa kundi upo kama ufuatavyo

1 Olympic Kalebia 6

2 . MTC 4

3 Nemo 2

4 Dicha 0

Chanzo: eatv.tv