Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MSF yatahadharisha kuhusu hali mbaya nchini Sudan

Baraza La Usalama La Umoja Wa Mataifa Lataka Wanajeshi Kuuachilia Mji Wa El Fasher Sudan MSF yatahadharisha kuhusu hali mbaya nchini Sudan

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), imefichua baadhi ya majanga ya binadamu yaliyosababishwa na vita kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwa raia yakiwemo mauaji, mateso na ukatili wa kingono, huku mapigano yakiendelea kati ya pande hizo mbili katika maeneo kadhaa ya Sudan.

Katika ripoti yake iliyopewa jina la "Vita dhidi ya Mwanadamu - Gharama ya Migogoro na Ukatili nchini Sudan," Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka limesema kwamba vikosi vya jeshi la Sudan na vya wapiganaji wa RSF na wafuasi wao vinatenda ukataili wa kutisha kwa watu kote nchini.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa, vita vya Sudan vimesababisha kuporomoka kwa ulinzi wa raia, na jamii za wenyeji zinakabiliwa na ukatili wa kiholela, mauaji, mateso na unyanyasaji wa kingono huku mashambulizi yakiendelea dhidi ya wahudumu wa afya na vituo vya matibabu.

Ripoti hiyo imewasilisha ushuhuda wa wahudumu wa afya na watu walionusurika ambao wamesimulia mambo ya kutisha waliyoshuhudia wakati wakikimbia jahanamu ya vita kuelekea maeneo mengine.

Ripoti ya MSF imesema, hospitali zinaporwa mara kwa mara na kushambuliwa wakati wote wa vita.

Siku chache zilizopita, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilitangaza kwamba zaidi ya Wasudan milioni 10 wamekimbia kutoka miji na vijiji vyao tangu kuanza vita vya ndani mwezi Aprili 2023, huku njaa ikiendelea kuathiri raia wengi wa nchi hiyo.

Sudan IOM ilisema kuwa nusu ya wakazi wa Sudan yaani karibu watu milioni 50 wanakabiliwa na janga la njaa na wanahitaji misaada ya kibinadamu kuliko nchi nyingine yoyote duniani.

Sudan imelitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe baina ya pande mbili zinazoongozwa na majenerali wa jeshi katikati ya mwezi wa Aprili 2023, na juhudi za kusuluhisha baina ya pande mbili hazijazaa matunda hadi sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live