Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Licha ya ukame, Ronaldo anaanza

Cr Ronaldo Licha ya ukame, Ronaldo anaanza

Sat, 5 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Ralf Rangnick anatarajiwa kusimama na Cristiano Ronaldo na atamuanzisha fowadi huyo katika mchezo wa Manchester Dabi, Jumapili dhidi ya Manchester City, kwa mujibu wa taarifa.

Awali, Ronaldo alianza maisha yake vyema Old Trafford akifunga mabao nane katika mechi zake 15 za kwanza za ligi, huku pia akifanya kazi kubwa kuisaidia United kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, tangu kuanza kwa mwaka huu, mabao yake yamekauka akiwa amefunga bao moja tu katika mechi 10 zilizopita za michuano yote.

Katika mchezo wake wa hivi karibuni dhidi ya Watford, Ronaldo alikosa nafasi kibao United ilipobanwa kwa suluhu Old Trafford.

Ubutu wake langoni umeanza kuwafanya baadhi wahoji kama atapata nafasi dhidi ya Manchester City, lakini taarifa ya The Sun inaeleza kuwa Rangnick atamuanzisha kwenye first eleven.

Inaelezwa kuwa Rangnick anaamini Ronaldo, 37, aliyewekwa benchi dhidi ya Burnley mwezi uliopita, atakuwa amenufaika na mapumziko ya siku nane kabla ya kuivaa City.

Kwa sasa United wapo nafasi ya nne kwenye msimamo lakini wamejikuta wapo pointi mbili tu mbele ya Arsenal walio na viporo vitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live