Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#KombeLaDunia2022: Afrika Kusini yataka mchezo wa marudiano na Ghana

Eywter #KombeLaDunia2022: Afrika Kusini yataka mchezo wa marudiano na Ghana

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: BBC

Shirikisho la Soka la Afrika Kusini (Safa) linatarajiwa kwasilisha malalamishi rasmi kwa Shirikisho la Soka Duniani FIFA kuhusu uchezeshaji wa mwamuzi katika mechi yao ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Ghana Jumapili usiku.

Ikihitaji sare ili kufika raundi ya tatu na ya mwisho ya kufuzu kwa Afrika, Afrika Kusini ilipoteza 1-0 baada ya Ghana kupiga penalti iliyozua utata.

Ushindi huo mdogo wa Black Stars uliwawezesha kufuzu kwa hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia la Afrika kwa tofauti ndogo, na kuwaondoa Afrika Kusini kileleni mwa kundi hilo kwa idadi ya mabao.

Mkwaju huo wa penalti ulitolewa baada ya kiungo wa Leicester City na Ghana, Daniel Amartey kuanguka kufuatia kile kinachosemekana kugongwa kidogo na mlinzi Rushine de Reuck, ambaye alilishwa kadi kwa ajili ya kosa hilo.

"Tutawaandikia Caf [Shirikisho la Soka la Afrika] na Fifa - kwanza kuchunguza jinsi mchezo ulivyoendeshwa na pili kupinga baadhi ya maamuzi haya," Mkurugenzi Mtendaji wa Safa Tebogo Mothlante alisema Jumatatu.

"Kama tulivyofanya jana usiku, tayari tumemfahamisha kamishna wa mechi kwamba tutawasilisha malalamiko rasmi."

Chanzo: BBC